Home » Maisha & Mapenzi » Jinsi ya kumfikisha mwanamke kileleni
Jinsi ya kumfikisha mwanamke kileleni

Jinsi ya kumfikisha mwanamke kileleni

Mwili wa mwanamke ni tofauti na wa mwanaume linapokuja swala la kujamiiana. Mwanaume ni rahisi sana kupata ashki hasa akiona mwili wa mwanamke ukiwa uchi. Mwanaume anachohitaji ili apate ashki ni kuwaza ngono, pamoja na kuona mwili wa mwanamke, hiyo inatosha kumuweka tayari kwa tendo la kujamiiana. Kwa kawaida mwanaume huwa anapata ashki kwenye maeneo yake ya siri peke yake na siyo mwili mzima kama ilivyo kwa mwanamke.

Mwanamke yeye ili aweze kupata ashki na awe tayari kufanya tendo, inatakiwa aandaliwe vya kutosha, kwani mwili wake wote unatakiwa upate ashki na siyo sehemu zake za siri peke yake kama ilivyo kwa mwanaume. Kuamsha sehemu za siri za mwanaume ni rahisi sana, ni eneo dogo, na huchukua muda mfupi sana, chini ya dakika moja. Lakini kuamsha mwili wa mwanamke ili uwe tayari kufanya ngono siyo rahisi kufanya hicho, inahitaji muda mrefu, zaidi ya dakika tano mpaka saa moja au zaidi kutegemea aina ya maandalizi au aina ya mwanamke. Kwa hiyo wanaume wanatakiwa wafahamu tofauti hizi, ili kupunguza lawama zipungue kama sio kuzifuta kabisa.

Kwa kawaida baadhi ya wanaume huwa wana haraka sana na papara sana, na sijui huwa wanataka kuwahi nini na wapi. Mwanaume huwa hana subira wakati wa kufanya ngono, anataka afanye haraka, amalize kisha ageukie ukutani. Sijui huko ukutani huwa kuna nini, huu ni ukatili, haukubaliki. Haitakiwi mwanaume amwingilie mwanamke kama mwanamke hajawa tayari kwa tendo. Maandalizi kabla ya ngono ni jambo muhimu sana kuliko hata ngono yenyewe. Kama maandalizi yakiwa mazuri utaifurahiya ngono, lakini maandalizi yakiwa hafifu huwezi kuifurahia ngono. Kuna njia nyingi sana za kumuandaa mwanamke, nitazitaja chache. Mojawapo ni njia ya mazungumzo, mwanaume anatajkiwa aaongee na mpenzi wake kwa lugha nzuri, kwa maneno matamu na yenye mahaba. Atumie muda mwingi kuzungumza naye, asiwe na haraka kuanza kufanya ngono. Mazungumzo yahusu masuala ya uhusiano ukiwemo upendo. Usizungumzie madeni yako unayodaiwa, matatizo yako au ya familia yenu.

Baadhi ya wanwake wanaweza kujisikia kujamiiana kutokana na mazungumzo peke yake. Lakini pia kuna baadhi ya wanawake wengine ambao huwa hawapendi kufanya ngono. Unapokutana nao kwa mara ya kwanza, wanataka tu mzungumze tu na si zaidi ya hapo. Jambo hili kwa wanaume walio wengi ni gumu sana, wao wanataka ngono siku hiyo hiyo ya kwanza. Sisemi kufanya hivyo ni vibaya au vizuri, inategemea mazingira na makubaliano yenu. Njia ya pili ni ya kumshikashika sehemu mbalimbali za mwili wake. Njia hii inaweza kwenda sambamba na ile ya kwanza. Wakati unamshikashika usitumie nguvu, mshike kama vile unampapasa. Achana na mambo yote uliyoambiwa na rafiki zako kwamba mwanamke ukimshika sehemu fulani ndio anajisikia kufanya ngono. Wanwake wanatofautiana.

Linapokuja swala la kujamiiana mwili wa mwanamke unaweza kuufananisha na dunia hii tunayoishi. Una milima na mabonde, mito, maziwa na bahari, mbuga za wanyama n.k. Kwa kifupi ni kwamba, una kila kitu unachokiona hapa duniani, ni juu ya mwanaume kuwa mvumbuzi wa maeneo mbalimbali atakayoyatumia kumuandaa mwanamke aliye naye ili awe tayari kufanya ngono na kufika kileleni kwa urahisi. Wakati mwanaume anaendelea na utafiti huo wa kumuandaa mwanamke anatakiwa awe macho na atumie milango yake sita ya fahamu

Mwanaume anatakiwa atumie milango yote sita ya fahamu ili kujua ni maeneo gani anapoyagusa yanamfanya mwanamke ajisikie raha zaidi na kumfanya asisismke. Pia ni maeneo gani akiyagusa yanamfanya ajisikie vibaya. Mwanaume anatakiwa apeleke uzingativu wake kwenye yale maeneo yanayomfanya mwanamke ajisikie raha. Kwa kawaida, maeneo Fulani yanaweza yakamfanya mwanamke fulani ajisikie raha, lakini maeneo hayo hayo ukimshika mwanamke mwingine anajisikia vibaya au anakereka. Haitakiwi mwanaume akariri maeneo yanayoleta msisimko mmoja na kuyatumia kwa amwanamke mwingine. Kwa hiyo mwanaume anatakiwa aachane na mazoea, wakati wa kumuandaa mwanamke.

Kila siku mwanaume anatakiwa ahakikishe anavumbua maeneo mapya, milima mipya, mito mipya, mbuga mpya, bustani mpya, bahari mpya n.k. Nilisema mwili wa mwanake ni kama dunia, hivyo mwanume hatakiwi atosheke na maeneo aliyoyagundua, kila siku anatakiwa agundue maeneo mapya yanayoleta msisimko kwa mwenzi wake.

Je utajuaje kwamba sasa mwanamke yupo tayari kwa tendo?
Baadhi ya dalili utakazoziona ni mabadiliko katika upumuaji, sehemu zake za siri, matiti, kijasho chembamba kwenye ngozi n.k. Lakini kwa kuwa wewe ni mvumbuzi, hakikisha unavumbua nyingine nyingi zaidi. Ukweli ni kwamba zipo nyingi mno, usikariri, kila mwanamke ana dalili zake, kuna uwezekano mkubwa zikatofautiana. Baada ya kuona dalili hizo, ndipo tendo linaweza kufanyika.

Kufika kileleni
Jambo la kwanza litakalokuwezesha kufika kileleni ni kufuta kwenye akili yako yale mambo yote hasi uliyoambiwa na jamii kwamba ngono ni mbaya, ngono ni uchafu n.k.

Jambo la pili ni kutoruhusu akili yako kuingilia wakati unafanya ngono. Kama kitanda kinapiga kelele, kiache kipige kelele. Kama unajisikia kulia wakati unafanya ngono usijizuie, bali lia. Ukijisikia kupiga makelele, piga, usijizuie. Kama utajisikia kunyanyua miguu juu au mikono, usijizuie, we nyanyua tu. Uache mwili ufanye chochote unachotaka kufanya. Usiiruhusu akili yako kuingilia kwa namna yoyote wakati unafanya ngono. Usiwe mshiriki na badala yake unatakiwa uwe mtazamaji. Unatakiwa uwe mshuhudiaji wa mwili wako na tendo lote kwa ujumla. Uwe kama mtu anayetazama mpira uwanjani na siyo mchezaji.

Wakati unaendelea na ngono usiiruhusu akili yako ikaanza kuwaza kwamba, huyu mpenzi uliye naye ni mzuri au mbaya, anajua mapenzi au hajui, leo nitafaidi au sitafaidi, sijui nitamridhisha, sijui nitaambukizwa ukimwi au magonjwa ya zinaa, sijui nitapata mimba, sijui kondom itapasuka, sijui kuna watu wanatuchungulia huko nje, sijui haya maumbile yake makubwa yataniumiza n.k. Akili yako inatakiwa ijiepushe na mawazo ya aina hiyo au yanayofanana na hayo.

Kama akili yako imejaa mawazo ya aina hiyo, ni vigumu sana kufika kileleni. Ukweli ni kwamba huwezi kufurahia ngono hata kidogo, sana sana utatoa manii tu basi.

About Bongo Lifestyles Editor

Bongo Lifestyles Editor

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*

You may use these HTML tags and attributes: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <strike> <strong>

Scroll To Top